AzamPesa ni mtoa huduma wa pesa za kieletroniki ambaye hutumia pochi za kidijitali kuruhusu wateja wake kutuma na kupokea fedha, kufanya malipo ya bidhaa na huduma kama AzamTV, kununua tiketi za AzamFerry, malipo ya Serikali, MasterCard QR na kutoa pesa kutoka kwenye pochi zao.
AzamPesa inapatikana katika mitandao yote ya simu. Kama una simu janja unaweza kupakua App ya AzamPesa kupitia Google Playstore au App store kwa watumiaji wa iOS. AzamPesa pia inapatikana kiurahisi kwa kupiga *150*08# na utaweza kupata huduma zote.