Jeshi la Polisi la Tanzania lilianzishwa rasmi 25 August 1919 kwa tangazo la Serikaliya Kiingereza lililotoka Gazeti la Serikali No.Vol.1 No.21-2583 kwa wakati huo likaitwa Jeshi la Polisi Tanganyika. Lakini jeshi lilianzishwa kisheria kwa Sheria ya uanzishajiwa Jeshi la Polisi ya mwaka 1939 [THE POLICE FORCE AND AUXILIARY SERVICES ACT OF 1939) PRINCIPAL LEGISLATION. Sheria hii ndiyo inatumika hadi sasa japo imekuaikifanyiwa marekebisho ya mara kwa mara.